Baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu, muimbaji aliyewahi kutamba
nchini, Buibui amerejea tena akiwa chini ya uongozi mpya wa Tanzania
Music Power, TMP.
Latest info ni kwamba TMP ambayo ni jumuia mpya ya mapinduzi iliyoingia rasmi katika
kuokoa kizazi cha muziki wa Bongo Fleva Tanzania imeingia makubaliano na
msanii huyo ambaye jina lake ni Frank Lewis Katende Kivunike.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari TMP imesema imeingia
makubaliano na Buibui baada ya kukiona kipaji chake na juhudi zake
katika kufanya kazi ya muziki wa kizazi kipya.Kwa hiyo wale mashabiki wake wakae mkao wa kumpokea upya katika tasnia hii ya Bongo Flevaa!!!!!!!!!!!!!!!!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment