Pages

Interview Sessions!!

My blog is basically about entertainment news. Events, exclusive stories, hot gossip and the everyday life of your very own bongo superstars! Music artists, film artists, producers, models, fashion designers, you name it.. one on one interviews and full coverage of events!

Interview Sessions!!

National Stadium for Bongo Flava vs Bongo Movies Soccer Match.

Interview Sessions!!

Nigerian actress Omotola Jalade .

Interview Sessions!!

Kanumba’s mother, on the Thanksgiving mass of his death.

Interview Sessions!!

Jose Chameleone and Mario Van Peebles at ZIFF 2012, Zanzibar

Thursday, December 20, 2012

TUESDAY KIHANGA KUTOKA NA TAMTHILIA MPYA MWAKANI

Muongozaji na muingizaji wa filamu za hapa nchini maarufu kama Tuesday Kihanga a.k.a Mr Chuzi mwaka amejipanga upya na anatarajia kutoka na filamu mpya inayokwenda kwa jina la High Heels.Katika filamu imehusisha wasanii mbalimbali mastaa kama Kojack, Jini Kabula,Badi,Kishoka na Rayuu bila kusahau wengineo wazuri.Kwa hiyo kama wewe ni shabiki wa filamu kaa tayari kwa ujio mpya wa filamu hiyo.

UJUMBE KUTOA KWA SUGU KUHUSU HOSPITAL YA RUFAA MKOANI MBEYA HUU HAPA

Msanii mkongwe wa Hip-Hop maarufu kama Sugu hapa nchini baada ya kutamba na baadhi ya ngoma zake kama Mchaka Mchaka, Hayakuwa Mapenzi, Sugu na Hakuna Matata, Mr. II ambae pia ni anafahamika kama Mheshimiwa Joseph Mbilinyi leo kupitia katika ukurasa wake wa facebook inaonyesha kwamba amekerwa na tabia za madaktari wa mkoa wa Mbeya kwa kujali sana rushwa kuliko utu wa watu.
        Sugu ameonesha kukerwa huko pale alipoandika kupitia ukurasa wake wa Facebook na kusema kuwa madaktari wa Mbeya, katika hospitali ya rufaa wamekuwa wakiwaweka wagonjwa POP kwa kiasi cha gharama ya Tshs. 300,000/= hadi laki Tshs. 500, 000/= na kuonesha kuwa amechoshwa na kitendo hicho.
Soma alichoandika hapo chini:

REHMTULLAH ATAJA WEBSITE INAYOTUMIA JINA LAKE KATIKA KUTAPELI MA MODELING

Mbunifu wa hapa Tanzania maarufu kama Ally Rehmtullah leo kupitia katika ukurasa wake wa facebook aliweza kufunguka na kuweka mtandao ambao unapenda mara nyingi kutumia jina lake katika kutapeli ma modeling wa hapa Tanzania.
http://www.modelscooperation.wapka.mobi/index.html

Q CHILLAH AMEKIRI KUWA ALIKUWA ANATUMIA MADAWA YA KULEVYA ASEMA "I 'M RESPONSIBLE FOR MY FAILURE"

Muimbaji Abubakar Katwila a.k.a Q Chillah amekiri kuwa alikuwa mtumiaji wa madawa ya kulevya takribani miaka miwili iliyopita lakini kwasasa ameachana nayo na ana miezi saba toka aache.sisi kama member wa E-BIZZ 255 tunakupa big up broo kwa uamuzi wako.

BARNABA,SUMA LEE,BABU TALE WAMEWASILI LONDON

Suma Lee,Babu Tale na Barnaba baada ya kuwasili London kwa ajili ya kupiga show yao ambayo inatarajia kufanyika siku ya tarehe 22 mwezi huu huko london,sasa waliweza kukaribishwa katika ofisi za BBC Swahili kwa ajili ya interview na mtangazaji Charles Hillary huko London.

UJUMBE KUTOKA FLAVIANA MATATA FOUNDATION

   Flaviana Matata Kupitia FMF maarufu kama Flaviana Matata Foundation inawatakia watu wote heri ya Christmas na Mwaka Mpya 2013 na mapumziko mema katika kipindi hiki cha mapumziko na likizo fupi.

Wednesday, December 12, 2012

NO NAME GROUP KUACHIA NGOMA YAO MPYA"HAND UP"

No name The Group ni kundi jipya ambalo limehusisha ma producer wakali ambao walifanya vizuri katika sanaa ya muziki hapa Tanzania na bado wanaendelea kufanya vizuri ambao ni Dunga,P Funk,Karabani,Lamar na John Mahundi,sasa basi leo  wameachia rasmi ngoma yao mpya inayokwenda kwa jina la Hands Up katika vituo mbalimbali.

 

Blogger news

Blogroll

About