Pages

Thursday, July 26, 2012

WOLPER ATENGENEZA FILAMU KWA GHARAMA KUBWA


Imeelezwa kuwa  wasanii wengi wa kibongo wanapotengeza filamu zao ni chini ya milioni 7, lakini mmoja wa  wasaniiwa filamu bongo Jackline Wolper, inadaiwa kuwa ni nyota pekee anayetengeneza filamu kwa gharama kubwa kuliko msanii yeyote Tanzania.

Chanzo kiomja cha habari kimeeleza kuwa  msanii  huyo hutumia sh mil 25-30 katika filamu moja kiasi ambacho hakuna msanii yeyote anaefikia.

Wasanii wengi wa kibongo hutengeneza filamu kwa mil 5-7, ingawa kiasi hicho ni kikubwa, kwani hata wale wasanii wanaoshiriki katika filamu hizo, wanalipwa kaisi kidogo cha pesa.

“Wolper amekuwa msanii namba moja katika kutengeneza filamu za gharama, na pesa hizo zinatumia katika malipo ya wasanii, hivyo unazani kama angekuwa anatumia mil 7, katika kutegeneza filamu hata hao wasanii wanaoshiriki watalipwa kiasi gani,” Kilisema chanzo hicho.

Chanzo hicho Kiliongeza kuwa  wapo baadhi ya waandaaji wa filamu wengine ambao huwalipa wasanii sh 50,000 na kiwango cha juu sana ni sh laki moja ‘100,000' lakini kwa upande wa Wolper huwalipa kiasi kikubwa cha pesa wale wanaoshiriki katika filamu zake.

0 comments:

Post a Comment

 

Blogger news

Blogroll

About