Chanzo kiomja cha habari kimeeleza kuwa msanii huyo hutumia sh mil 25-30 katika filamu moja kiasi ambacho hakuna msanii yeyote anaefikia.
Wasanii wengi wa kibongo hutengeneza filamu kwa mil 5-7, ingawa kiasi hicho ni kikubwa, kwani hata wale wasanii wanaoshiriki katika filamu hizo, wanalipwa kaisi kidogo cha pesa.
“Wolper amekuwa msanii namba moja katika kutengeneza filamu za gharama, na pesa hizo zinatumia katika malipo ya wasanii, hivyo unazani kama angekuwa anatumia mil 7, katika kutegeneza filamu hata hao wasanii wanaoshiriki watalipwa kiasi gani,” Kilisema chanzo hicho.
Chanzo hicho Kiliongeza kuwa wapo baadhi ya waandaaji wa filamu wengine ambao huwalipa wasanii sh 50,000 na kiwango cha juu sana ni sh laki moja ‘100,000' lakini kwa upande wa Wolper huwalipa kiasi kikubwa cha pesa wale wanaoshiriki katika filamu zake.
0 comments:
Post a Comment