Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imeshindwa kuendelea kusikiliza shauri la msanii wa filamu nchini Elizabert Michael ‘Lulu’ kutokana na jaji anayesikiliza kesi hiyo kuwa na majukumu mengine ya kikazi
Kesi hiyo iliyopo mbele ya jaji Dkt. Fauz Twaib alikuja kwa ajili ya kutajwa na iliahirishwa na msemaji wa mahakama hiyo Amiri Msumi Msumi alidai kuwa jaji anayesikiliza shauri hilo ni mwenyekiti wa Bodi za kodi na pia ni mwalimu wa sheria ya chuo kikuu Dar es Salaam , kutokana na hali hiyo shauri hilo limeahirishwa hadi Agosti 20 mwaka huu, Mara ya mwisho Jaji Twaib aliuleza upande wa mashtaka kuwa jalada la kesi hiyo limiitwa Mahakama Rufaa hivyo wahakikishe jalada hilo linapelekwa, kesi hiyo ipo Mahakama kuu kutokana na mawakili wanaomtetea msanii huyo akiwemo Peter Kibatala kuwasilisha maombi ya kutaka umri wa msanii huyo uchunguzwe Lulu anakabiliwa na kesi ya mauaji ya msanii mwenzake Steven Kanumba yanayodaiwa kufanyika Aprili 7, mwaka huu Sinza jijini Dar es Salaam
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment