Pages

Monday, July 30, 2012

FEZZA KESSY IS BACK!

Hivi mnakumbuka the adorable miss dar city centre who was also miss Ilala 2005? this girl made tones of headlines because kwa mwaka huo ushindani ulikuwa mkubwa sana miss tz, ukizingatia yeye ni mdogo wa miss tanzania 1997 Saida , people expected her to take home the crown. alisimama stage moja na warembo kama nancy sumari which made it even more exciting...

   that beautiful smile is back kwenye limelight, na sasa ameamua kujikita kwenye muziki na yupo THT akifanya training za sauti. she says anatamani sana kufanya kazi na Diamond, anapenda his charm and stage performance. she has a beautiful baby boy, amabe alimpata during the time that she was living in UK where she went a few months after miss tanzania to do a degree in business administration.
And here's a clip of an interview that i did with her about the plans she has on her music career..

MSISHANGAE NIKIFANYA COLLABO NA FALLY IPUPA, D'BANJ AU HATA P'SQUARE


Barnaba is expected to tour in different countries in Europe and most especially jijini London, UK kwaajili ya tamasha la kusaidia nchi mbalimbali za Africa zilizokumbwa na janga la malaria. Atatembelea nchi kama Germany, Italy na France.
    What people dont know is that Barnaba amepata nafasi hii kutokana  na kupigiwa debe na Fally Ipupa. Waliwahi kufanya wote kazi, na Fally alipenda sana nidhamu ya kazi ya Barnaba pamoja na moyo wake wa kujifunza na kujituma, this is why ilikuwa raahisi  kwake kumpendekeza Barnaba straight away kushiriki kwenye tour hii.


   Anyways, anasema he is very happy kuwa the only artist from bongo ambae atashiriki kwenye Africa Unplugged tour huko Wembley arena, London, na pia mtarajie lots and lots of surprises kutoka kwake because he s gonna be there for 15 whole days na atakaa bweni moja na artists kama D'banj, Fally Ipupa, na wengine wengi so msishangae akifanya collabo na any of those artist.
   Big up Barnaba Boy.. we wish you all the best
  

Barnaba Boy Africa Unplugged Tanzania

'SIJAIBA WASANII KUTOKA BAND ZINGINE'-ANETH KUSHEBA

Akiwa amehusishwa na wizi wa waimbaji kutoka bendi mbalimbali, Aneth Kusheba amedai kuwa yeye amepewa tu jukumu la kuongoza skylight band na hivyo ametoa platform ya ajira mbambali kwa vijana, mainly band vocalists. so kama wamaeamua kuhamia skylight, ni kwasababu ya benefits wanazopata na sio vingine. pengine wamevutiwa na maslahi, or better working enviroments.. who knows?

       Although Banana Zorro wa B Band alisema Aneth aliachishwa kazi B bad kutokana na utovu wa nidhamu, she claims that she saw a better opportunity out there and she took it. It should not be understood otherwise.

Thursday, July 26, 2012

WOLPER ATENGENEZA FILAMU KWA GHARAMA KUBWA


Imeelezwa kuwa  wasanii wengi wa kibongo wanapotengeza filamu zao ni chini ya milioni 7, lakini mmoja wa  wasaniiwa filamu bongo Jackline Wolper, inadaiwa kuwa ni nyota pekee anayetengeneza filamu kwa gharama kubwa kuliko msanii yeyote Tanzania.

Chanzo kiomja cha habari kimeeleza kuwa  msanii  huyo hutumia sh mil 25-30 katika filamu moja kiasi ambacho hakuna msanii yeyote anaefikia.

Wasanii wengi wa kibongo hutengeneza filamu kwa mil 5-7, ingawa kiasi hicho ni kikubwa, kwani hata wale wasanii wanaoshiriki katika filamu hizo, wanalipwa kaisi kidogo cha pesa.

“Wolper amekuwa msanii namba moja katika kutengeneza filamu za gharama, na pesa hizo zinatumia katika malipo ya wasanii, hivyo unazani kama angekuwa anatumia mil 7, katika kutegeneza filamu hata hao wasanii wanaoshiriki watalipwa kiasi gani,” Kilisema chanzo hicho.

Chanzo hicho Kiliongeza kuwa  wapo baadhi ya waandaaji wa filamu wengine ambao huwalipa wasanii sh 50,000 na kiwango cha juu sana ni sh laki moja ‘100,000' lakini kwa upande wa Wolper huwalipa kiasi kikubwa cha pesa wale wanaoshiriki katika filamu zake.

MAHAKAMA KUU IMESHINDWA KUSIKILIZA SHAURI LA LULU

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imeshindwa kuendelea kusikiliza shauri la msanii wa filamu nchini Elizabert Michael ‘Lulu’ kutokana na jaji anayesikiliza kesi hiyo kuwa na majukumu mengine ya kikazi
Kesi hiyo iliyopo mbele ya jaji Dkt. Fauz Twaib alikuja kwa ajili ya kutajwa na iliahirishwa na msemaji wa mahakama hiyo Amiri Msumi Msumi alidai kuwa jaji anayesikiliza shauri hilo ni mwenyekiti wa Bodi za kodi na pia ni mwalimu wa sheria ya chuo kikuu Dar es Salaam , kutokana na hali hiyo shauri hilo limeahirishwa hadi Agosti 20 mwaka huu, Mara ya mwisho Jaji Twaib aliuleza upande wa mashtaka kuwa jalada la kesi hiyo limiitwa Mahakama Rufaa hivyo wahakikishe jalada hilo linapelekwa, kesi hiyo ipo Mahakama kuu kutokana na mawakili wanaomtetea msanii huyo akiwemo Peter Kibatala kuwasilisha maombi ya kutaka umri wa msanii huyo uchunguzwe Lulu anakabiliwa na kesi ya mauaji ya msanii mwenzake Steven Kanumba yanayodaiwa kufanyika Aprili 7, mwaka huu Sinza jijini Dar es Salaam
 

Blogger news

Blogroll

About