Pages

Thursday, December 20, 2012

TUESDAY KIHANGA KUTOKA NA TAMTHILIA MPYA MWAKANI

Muongozaji na muingizaji wa filamu za hapa nchini maarufu kama Tuesday Kihanga a.k.a Mr Chuzi mwaka amejipanga upya na anatarajia kutoka na filamu mpya inayokwenda kwa jina la High Heels.Katika filamu imehusisha wasanii mbalimbali mastaa kama Kojack, Jini Kabula,Badi,Kishoka na Rayuu bila kusahau wengineo wazuri.Kwa hiyo kama wewe ni shabiki wa filamu kaa tayari kwa ujio mpya wa filamu hiyo.

UJUMBE KUTOA KWA SUGU KUHUSU HOSPITAL YA RUFAA MKOANI MBEYA HUU HAPA

Msanii mkongwe wa Hip-Hop maarufu kama Sugu hapa nchini baada ya kutamba na baadhi ya ngoma zake kama Mchaka Mchaka, Hayakuwa Mapenzi, Sugu na Hakuna Matata, Mr. II ambae pia ni anafahamika kama Mheshimiwa Joseph Mbilinyi leo kupitia katika ukurasa wake wa facebook inaonyesha kwamba amekerwa na tabia za madaktari wa mkoa wa Mbeya kwa kujali sana rushwa kuliko utu wa watu.
        Sugu ameonesha kukerwa huko pale alipoandika kupitia ukurasa wake wa Facebook na kusema kuwa madaktari wa Mbeya, katika hospitali ya rufaa wamekuwa wakiwaweka wagonjwa POP kwa kiasi cha gharama ya Tshs. 300,000/= hadi laki Tshs. 500, 000/= na kuonesha kuwa amechoshwa na kitendo hicho.
Soma alichoandika hapo chini:

REHMTULLAH ATAJA WEBSITE INAYOTUMIA JINA LAKE KATIKA KUTAPELI MA MODELING

Mbunifu wa hapa Tanzania maarufu kama Ally Rehmtullah leo kupitia katika ukurasa wake wa facebook aliweza kufunguka na kuweka mtandao ambao unapenda mara nyingi kutumia jina lake katika kutapeli ma modeling wa hapa Tanzania.
http://www.modelscooperation.wapka.mobi/index.html

Q CHILLAH AMEKIRI KUWA ALIKUWA ANATUMIA MADAWA YA KULEVYA ASEMA "I 'M RESPONSIBLE FOR MY FAILURE"

Muimbaji Abubakar Katwila a.k.a Q Chillah amekiri kuwa alikuwa mtumiaji wa madawa ya kulevya takribani miaka miwili iliyopita lakini kwasasa ameachana nayo na ana miezi saba toka aache.sisi kama member wa E-BIZZ 255 tunakupa big up broo kwa uamuzi wako.

BARNABA,SUMA LEE,BABU TALE WAMEWASILI LONDON

Suma Lee,Babu Tale na Barnaba baada ya kuwasili London kwa ajili ya kupiga show yao ambayo inatarajia kufanyika siku ya tarehe 22 mwezi huu huko london,sasa waliweza kukaribishwa katika ofisi za BBC Swahili kwa ajili ya interview na mtangazaji Charles Hillary huko London.

UJUMBE KUTOKA FLAVIANA MATATA FOUNDATION

   Flaviana Matata Kupitia FMF maarufu kama Flaviana Matata Foundation inawatakia watu wote heri ya Christmas na Mwaka Mpya 2013 na mapumziko mema katika kipindi hiki cha mapumziko na likizo fupi.

Wednesday, December 12, 2012

NO NAME GROUP KUACHIA NGOMA YAO MPYA"HAND UP"

No name The Group ni kundi jipya ambalo limehusisha ma producer wakali ambao walifanya vizuri katika sanaa ya muziki hapa Tanzania na bado wanaendelea kufanya vizuri ambao ni Dunga,P Funk,Karabani,Lamar na John Mahundi,sasa basi leo  wameachia rasmi ngoma yao mpya inayokwenda kwa jina la Hands Up katika vituo mbalimbali.

MISS TANZANIA 2012 BRIGITTE ALFRED AKABIDHIWA RASMI NOAH

 Brigitte Alfred,Redds Miss Tanzania 2012 akabidhiwa zawadi ya gari yake rasmi na katibu mkuu wa kamati ya Miss Tanzania Bw.Bosco Majaliwa katika ofisi ya Lino International Agency Limited zilizopo mikocheni jijini Dar es Salaam.



FLAVIAN MATATA ASHINDA TUZO YA FACE OF AFRICA

Mwanamitindo kutoka hapa Tanzania maarufu kama Flavia Matata, siku ya jumamosi iliyopita ameweza kuibuka kuwa mshindi wa tuzo za Face of Africa.Mashindano ya tuzo hizo yalifanyika katika mji wa New York Nchini Marekani.Tuzo hizo utolewa kwa kuwapongeza wa Africa ambao hufanya vizuri katika kazi zao.

CHEGGE SOON KUANZA KUINGIZA MOVIE YA MWANAYUMBA

Msanii wa Bongo Fleva almaarufu kama Chegge Chigunda anayekubalia hapa Tzee mpaka East Africa kwa ngoma zake kali kama Mwanayumba,Kinomanoma,Mikanda,Mkono mmoja na ngoma nyingine kali sasa
Latest Info kutoka kwa msanii huyu ni kwamba aliamua kuweka wazi kwamba kwa sasa japokuwa  wameshatoka ngoma yao mpya ya kundi inayokwenda kwa jina la Tutaonekanaje na wameshaitoa katika vituo mbalimbali sasa habari nzuri nyingine kutoka katika kundi ili ni kwamba wamepanga mikakati ya kufanya movie yao mpya inayokwenda kwa jina la Mwanayumba.Kwa hiyo wale mashabiki wa Tmk Wanaume Family dzain kama inawahusu hii.

JANA RAY-C-AMTEMBELEA-RAIS-KIKWETE-KUMSHUKURU-KWA-MSAADA

Mwanamuziki wa Bongo Fleva maarufu kama Ray C siku ya leo amemtembelea Rais Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam na kumshukuru kwa msaada wa matibabu kipindi alipokuwa mgonjwa.

Tuesday, December 11, 2012

BHOKE ATEULIWA KUWA BALOZI WA TAASIAI YA KUPAMBA NA FUNZA ZA MIGUUNI

mwakilishi wa Tanzania katika shindano la Big Brother Africa, 2011, Bhoke Egina ameteuliwa kuwa balozi mpya wa Tanzania wa taasisi ya Ahadi Trust Tanzania.


Mshindi wa BBA 2007, Richard, Bhoke Egina na Cecilia Mwangi wa Ahadi Kenya wakimhudumia mtoto aliyeathirika na funza...................................!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

LAMAR AJA NA UJIO MPYA WA KUNDI LAKE "MASHOSTIZI"

Producer kutoka katika Label ya Fishcrab Audio Station maarufu kama Lamar, siku zilizopita baada ya kutangaza katika vyombo mbalimbali vya habari kwamba anatafuta wasichana ambao wenye uwezo wa kuimba ili aweze kufanya nao kazi katika studio yake,hatimaye amefanikio kupata wasichana watatu ambao ni Nuru,Salma na Menyinah.Katika mazungumzo lamar alisema kwamba kwasasa kundi hilo limeshamaliza kutengeneza ngoma yao mpya ila wapo katika mchakato wa kuandaa video yao mpya chini ya Director Adamu juma.
 

Blogger news

Blogroll

About